Nandy afunguka alivyopata dili la kumvalisha Naibu Spika Dk Tulia Ackson

Msanii Nandy amefunguka njia aliyotumia mpaka alivyofanikiwa kupata dili la kumvalisha Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson.

Related image
Hitmaker huyo wa One Day, amesema baada ya kupata kazi ya ubalozi wa taasisi ya Tulia Trust ya kiongozi huyo hapo nido alipotafuta nafasi nyingine ya kuwaa karibu zaidi na Spika huyo na alimuomba amshonee nguo tano bure na kama atazikubali ataomba afanye naye kazi.
“Nilirudi nyumbani nikamchunguza nikasema huyu anavaa vitenge kila siku, anashonewa na nani? nikakaa nikasema sijamzoea lakini nikikutana naye kwenye matamasha mawili tu tukiongea tutaconnect,” amesema msanii huyo.

“Katika kuconnect naye nilimuuliza mama unavyalishwa na nani? Mimi ninamafundi wangu [alimjibu]. Nikamwambia mimi ninaomba nikushonee nguo tano bure halafu uniambie ukipenda mimi nitakuvalisha, and then I do it. Tumetoka Bagamoyo nguo aliyokuwa ameivaa nilikuwa nimemvalisha mimi. Na yeye ndio aliyefanya nikapata connection za wabunge wengine kuwavalisha,” ameongeza

Comments