Mwigizaji maarufu wa filamu za James Bond Roger Moore amefariki

Roger Moore amefariki baada ya kuugua saratani
Roger Moore amefariki baada ya kuugua saratani
Mwigizaji maarufu wa filamu za James Bond Roger Moore amefariki.
Katika taarifa ya familia yake marehemu iliochapishwa katika mtandao wake wa Twitter, walisema ''ni vigumu kutangaza kifo cha baba yetu Roger Moore ambaye amefariki nchini Switzerland baada ya kuugua saratani''.
Roger Moore ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 89 alirahisisha kazi ya James Bond , jukumu ambalo lilimfanya kuwa maarufu sana.
Ilianza filamu ya Sean Connery ya 007 na baadaye sardonic humor ambayo ilizua hisia nyingi.
Aliwahi kuwa mwigizaji aliyeigiza kwa kipindi kirefu katika filamu ya James Bond huku filamu zake 7 za Bond zikiuzwa sana.
Roger Moore alizaliwa mjini Stockwell kusini mwa mji wa Landon mnamo tarehe 14 Oktoba 1927 akiwa mwana wa afisa wa polisi.
Akiwa katika umri wa miaka 15 alienda chuo kikuu kabla ya kuwa mwanafunzi katika uhaishaji Studio ambapo alifurahia sana.

Comments