Mwigizaji Jamie Foxx aelezea alivyookolewa na Oprah


Mwigizaji mkubwa Marekani Jamie Foxx ameelezea jinsi Oprah na baadhi ya waigizaji weusi Marekani walivyomsaidia kuacha ulevi.

 Jamie anasema baada ya kuigiza filamu ya “Ray” alikuwa anaelekea kupotea kabisa kwenye tasnia ya filamu na kuharibu maisha yake kabisa kutokana na pombe na starehe za hovyo.
Jamie anasema Mwaka 2005 Oprah alinipigia simu na kunitahadharisha kuhusu tabia yangu ya starehe za hovyo, alinipeleka mahali kwaajili ya maombi kwenye nyumba ya Quincy Jones, kitu ambacho alikiita [come-to-Jesus moment] na hapo mwigizaji mkubwa Sidney Poitier na waigizaji wengine weusi walikuwepo, na walinishawishi niwe SOBER na niwe na maisha tofauti“…..
Jamie hajasema kama alienda SOBER house ila baadae alikuja kushinda tuzo kubwa ya Best Actor Oscar kwa filamu ya “Ray”.

Comments