Mwathiriwa wa mkasa wa moto
Mwathiriwa aliyechomeka ambaye anamnyonyesha mtoto wake wa pili licha ya uchungu anaoupitia , amesema anafanya hivyo kuwapatia matumaini wanawake wachanga.
Schamica Stevenson maarufu kama Mimi mwenye umri wa miaka 34, alichomeka vibaya akiwa na umri wa miaka miwili, kwenye moto uliozuka nyumbani katika jimbo la Michigan, nchini Marekani.Hakumnyonyesha kifungua mimba wake lakini mtoto wake wa pili aliamua kumnyonyesha.
''Nilitaka kusambaza habari hii kuwasaidia wengine kutokata tamaa, kama nilivyofanya nikiwa na miaka 20,'' alisema Schamica.
''Kama matiti yanafanya kazi , yanastahili kutumika jinsi yalivyoumba kufanya.''
Alimekuwa akifanyiwa upasuaji wa ngozi kwa wakati mwingi maishani mwake na amesema alikuwa na wasiwasi kubeba ujauzito kwa mara ya kwanza alipokuwa na miaka 20 kutokana na alama kwenye tumbo lake.
Mimi, ambaye kwa hivi sasa anafanya kazi kama mkaguzi msimamizi wa afya ,amesema mara ya kwanza hakuwa na wakati wa kunyonyesha lakini alitamani kujaribu kwa wakati huu.
Nilikuwa mdogo na sikuwa na uvumilivu wa kustahimili wakati huo wakati wa kumnyonyesha mtoto.
''Wakati huu nilitaka kunyonyesha.''
Mpiga picha wa Marekani Ivette Ivens, alizichapisha picha za Mimi kwenye ukurasa wake wa Facebook , akimtaja kama mama wa watoto wawili. Muathiriwa wa moto. Shujaa. Anayenyonyesha.
Amesema alikuwa na maziwa kidogo na ilimbidi kumnyonyesha mtoto wake na pampu na sirinji kabla ya kumpa mtoto titi.
''Muuguzi wa unyonyeshaji alinisaidia sana nilipokuwa hospitali ,'' anasema
Nilikamua maziwa baada ya saa tatu na baada ya kula nikiwa bado hospitali lakini nikaona kwamba sikuwa napata maziwa mengi bado''
Licha ya kuwa na alama za kuchomeka , Mimi anatumai picha zake zitahamasisha wanawake wengine kujinuvunia kwa miili yao.
Inanivunja moyo nikisikia mtu anajitoa uhai kutokana na sura zao,'' amesema na hapa mimi sijali lolote natembea kila mahali nikama mimi ni Beyonce au Tamar Braxton.
''Sikupata ujasiri kwa siku moja , lakini najivunia kuwa mjasiri kwa sasa.
'Kuna wakati nilijihisi mnyonge kwa sababu mimi ni binadamu , lakini narudi na kumshukuru Mungu kwa maisha yangu na watoto wangu niliweza kujifungua na kuwalea.''
Comments
Post a Comment