Muongozaji wa filamu ya ’12 Years a Slave’ kuandaa documentary ya Tupac

Muongozaji wa filamu ya 12 Years a Slave, Steve McQueen, anatarajia kuongoza documentary kuhusu maisha ya rapper Tupac aliyefariki Septemba 1996.

McQueen amesema anatarajia kushirikiana na familia ya rapper huyo kutayarisha documentary hiyo itakayokuwa inamuelezea Tupac kama mtu aliyekuwa na kipaji kikubwa.
“I am extremely moved and excited to be exploring the life and times of this legendary artist. I attended NYU film school in 1993 and can remember the unfolding hip-hop world and mine overlapping with Tupac’s through a mutual friend in a small way. Few, if any shined brighter than Tupac Shakur. I look forward to working closely with his family to tell the unvarnished story of this talented man,” amesema McQueen.
Documentary hiyo itatayarishwa kupitia kampuni mbili ikiwemo Amaru Entertainment ambayo ilianzishwa na Afeni Shakur ambaye ni mama yake Tupac aliyefariki mwaka jana na nyingine ni White Horse Pictures.
Wakati huo huo mwezi Juni mwaka huu inatarajiwa kutoka filamu ya ‘All Eyez On Me’ ya Tupac ambayo imesusubiriwa kwa muda mrefu. Kwenye filamu hiyo Demetrius Shipp ameigiza kama Tupac huku Danai Gurira akiigiza nafasi ya Afeni Shakur.

Comments