Msichana aliyevuta na kutumbukizwa ndani ya maji na sili nchini Canada anatibiwa kwa madawa ya antibiotic kutokana na hatari ya kuugua maambukizi hatari.
Hifadhi ya samaki ya Vancouver Aquarium inasema familia ya msichana huyo imewasiliana nayo baada ya wafanyakazi kuelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuugua kutokana na bakteria zinazokuwepo baad ya mtu kuumwa na simba wa baharini. Mara nyengine mtu huishia kukatwa kiungo kutokana na kuumwa huko.
Msichana huyo amepata jeraha lenye ukubwa wa inchi 4 wakati mnyama huyo alipomuuma, babake alilielezea shirika la habari la CBC News.
Hatahivyo amekana kwamba walikuwa wanajaribu kumlisha Sili huyo wa baharini.
Video inayomuonyesha akiumwa na kuvutwa kwa rinda lake katika eneo la kuegesha meli la Richmond, British Columbia, na baadaye akiokolewana babu yake, imesambazwa katika mitandao ya kijamii, na kuzusha baadhi ya watu kusema kwamba familia hiyo ilikuwa inawalishi sili baharini.
"Kulikuwa na mtu karibu nao aliyekuwa anawalisha sili," alisema babake, aliyejitambulisha kwa jina lake la pili pekee Lau, ili kuepuka kutambuliwa msichana huyo.
Lakini amekiri kwamba bini yake aliwakaribia sana wanyama hao wa baharini, aliposogea ili awaone vizuri.
"Hilo ni funzo kali alilopata ," alisema
Bakteria zinazokuwepo midomoni mwa sili hao zinaweza kusababisha mtu kuugua maumivu mabaya na kuishia kuwa katika hali mbaya kama kuvimba na kupiga wekundu kwa viungo mwilini.
Comments
Post a Comment