
Wasichana wa Chibok
Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria.
Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi.Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.
Wasichana 82 waliachiliwa huru ikiwa ni kati ya mazungumzo yalioafikiwa na shirika la ICRC.
Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao duru ziliambia BBC.

Kundi hilo pia limewateka maelfu ya raia wakati wa operesheni zao katika eneo hilo.
Inaaminika kwamba baadhi ya wale waliotekwa wameozwa wapiganaji na wamepata watoto nao.
Comments
Post a Comment