Mji wa Marawi nchini Ufilipino wavamiwa na IS

Sheria ya kijeshi iliwekwa kwenye kisiwa cha Mindanao kutokana na machafuko mjini Marawi
Sheria ya kijeshi iliwekwa kwenye kisiwa cha Mindanao kutokana na machafuko mjini Marawi
Serikali ya Ufilipino imesema mji ambao upo kusini mwa kisiwa cha Mindanao umevamiwa na wapiginaji wa kundi la Islamic state.
Kwa zaidi ya siku mbili,Wanajeshi wa nchi hiyo wamekua wakitekeleza mashambulizi ya anga katika mji wa marawi,ambao umevamiwa na wanamgambo wa IS. Mapambano hayo yalianza baada ya wanajeshi wa Serikali kuvamia nyumba moja ikimtafuta Isnilon Hapilon, Kiongozi wa IS nchini Ufilipino na kiongozi wa kundi la Abu Sayyaf.
 
Wanamgambo waliungana na wapiganaji kutoka Malaysia na Indonesia na wamewashika mateka takriban watu 11 kutoka kanisa katoliki.
Takriban wanajeshi na Polisi 40 wameuawa kwenye mapambano ya kurushiana risasi, ambayo yamesababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao.

Comments