Mifugo kutumika kupata mikopo Kenya

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini muswada utakaotoa fursa watu kutumia mali zao kupata mikopo
Rais Uhuru Kenyatta ametia saini muswada utakaotoa fursa watu kutumia mali zao kupata mikopo
               
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametia saini muswada unaowaruhusu wakopeshaji kutumia vifaa vya nyumbani mimea na mifugo ili kujipatia mikopo.
Sheria hiyo kwa jina Movable Property Security Acto 2017 inatotoa fursa kwa kuanzishwa kwa sajili ya kwa mali hiyo ambazo benki zinaweza kutumia kuthibitisha umiliki dhamana yake.
Sheria hiyo mpya inalenga kuwasaidia wateja wa benki wasio na magari na vyeti vye umiliki wa gari ama hata ardhi kupata mkopo.
Sheria hiyo inakuza uthabiti na uhakika kwa kutoa dhamana ya mali ,rais alisema muda mfupi baada ya kutangaza kwamba ametia saini muswada huo.
Benki zimekuwa zikikataa kutumia mali inayoweza kuhamishwa kama dhamana ya mkopo kutokana na ukosefu wa data ambayo wanaweza kutumia ili kudai mali hiyo.
Ngombe wanaweza kutumika kupata mkopo katika benki Kenya
Uidhinishaji wa sheria hiyo huenda ikaigharimu serikali kwa kuwa ni sharti iweke sheria kama vile thamani ya chini ya mali inayoweza kutumika kama dhamana.
Sheria hiyo pia itabainisha ni mali gani ambayo inafaa kutumika kama dhamana

Comments