Messi kukabiliana na kifungo cha miezi 21 jela kwa kukweka kodi

Messi analipwa Euro milioni 40 kwa mwaka
Messi analipwa Euro milioni 40 kwa mwaka
Mahakama kuu nchini Uhispania imethibitisha adhabu ya kifungo cha miezi 21 jela na faini ya dola za Marekani milioni 2.2 dhidi ya Lionel Messi kwa kosa la kukwepa kodi, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya nyota huyo wa soka kukata rufaa.
Messi alihukumiwa mwezi Julai mwaka 2016, lakini huenda hukumu hiyo ikaahirishwa kwani nchini Uhispania ni kawaida kwa makosa ya kwanza ambayo si jinai kuwa na hukumu ya chini ya miaka miwili.

Comments