Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri
Kikosi cha Mbeya City Fc , leo kinaanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Yanga uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Uhuru jumamosi hii.
Afisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amearfu kuwa jumla ya nyota 18 na viongozi 10 watakuwa kwenye msafara huo kwa ajili ya kuhakikisha City inafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi.Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu, tunataka kushinda na kupata matokeo muhimu kwenye mchezo wa jumamosi,tunafahamu Yanga African ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo halitupi hofu kwa sababu sisi pia tuna kikosi kizuri, tulipata matokeo duru ya kwanza na sasa tunakwenda Dar kuhitimisha dhamaira yetu ya kupata poiti sita msimu huu kutoka kwao
Akiendelea zaidi Ten alisema City imekuwa na wiki nne za kujindaa vizuri kukabiliana na Yanga kwa kufanya mazoezi mazito ikiwa ni pamoja na kucheza michezo zaidi ya mitano ya kirafiki ambayo imesaidia kuimarisha uwezo wa nyota wa kikosi kiuchezaji na kuwaongezea Morari ya kutaka kushinda kwenye uwanja wa Uhuru.
Comments
Post a Comment