MBASHA: SINA TATIZO NA MWANAUME ALIYEMUOA FLORA

Msanii wa muziki wa Injili Tanzania, Emmanuel Mbasha amefunguka kwa kudai kuwa hana tatizo na mwanaume ambaye amemuoa aliyekuwa mama watoto wake, Flora.
Muimbaji huyo amedai hata akikutana na mwanaume huyo hawezi kumfanya lolote maana huyo mtu hakuwahi kumuingilia katika ndoa yake.
“Jamaa ambaye amemuoa Flora sina shida naye, anaweza kuwa mtu ambaye ananihofia kuwa nikikutana naye naweza kumdunda,” alisema Mbasha.
Aliongeza, “Ila huyo jamaa mimi simchukii na wala simjui. Hajawahi kuniingilia kwenye issue yangu yoyote ya mapenzi ila mimi namchukia jamaa ambaye aliniingilia kwenye ndoa yangu ndiye mbaya wangu, na Watanzania wote wanamjua,”
Mbali na hilo Emmanuel Mbasha alisema kuwa Flora amemkimbia kutokana na maisha aliyoyachagua lakini si kwamba alikuwa hana pesa, kwani yeye pesa alikuwa nazo toka mwanzo.

Comments