Marekani yaongeza vikwazo kwa Iran juu ya utengenezaji wa nyuklia

Iran imeahidi kupunguza utengenezaji wa Nyuklia
Iran imeahidi kupunguza utengenezaji wa Nyuklia
Marekani imeamua kuongeza vikwazo kwa serikali ya Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.
Hatua hii inakuja licha ya Rais Donald Trump kushutumu sera za mtangulizi wake Barack Obama juu ya kukabiliana na suala hilo.
Wakati wa kampeni, Trump alitishia kufuta makubaliano hayo ambapo Iran ilikubali kupunguza kiasi chake.
Trump amesema vikwazo zaidi vinahitajika kupambana na utengenezaji wa silaha za nyuklia duniani.
Ameongeza kuwa Marekani itaweka pia vikwazo kwa maafisa pamoja na wafanya biashara kutoka China ambao wanahusishwa na mpango wa nyuklia wa Iran.

Comments