
Picha ya gereza hilo iliyopigwa kwa Satelite
Marekani imeituhumu serikali ya Syria kwa kujenga sehemu ya kuchoma maiti katika jela ya kijeshi iliyopo karibu na Damascus ili kuficha mauaji ya halaiki ya wanaoshikiliwa na serikali.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeonyesha picha zilizopigwa kupitia njia ya Satelite ambazo imesema ni sehemu ya kuchoma maiti katika gereza lililopo Sednaya ambapo Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema maelfu ya wafungwa wameteshwa na kunyongwa. 
Ameongeza kusema kuwa, mauaji hayo yanafanyika kutokana Syria kuungwa mkono na Urusi na Iran.
Comments
Post a Comment