MAPACHA WA MARIAH CAREY NA NICK CANNON WAZIDISHA MAPENZI YA WAZAZI WAO

Ikiwa ni muda sasa tangu waachane na kila mtu kuamua kuendelea na maisha yake, hivi ndivyo sasa mambo yalivyo kwa Mariah Carey na Nick Cannon.

Maria na Nick wameonekana wakifurahi wakiwa na mapacha wao, Morocco na Monroe, kama familia moja katika siku hiyo muhimu kwa watoto wao waliotimiza miaka sita siku ya jumapili.

Katika kuadhimisha siku hiyo ya kuzaliwa kwa mapacha hao, iliyofanyika Disneyland mjini Marekani, Mariah na Nick walitumia muda wao mwingi kusherekea na watoto wapo huku wakinunuliwa keki mbili kwa kila mmoja,Zawadi za Computer na vitu vingi vya thamani.
Hatujashtuka kuona Maria na Nick kusherekea huko kwani ndio sehemu ambayo inasemekana mahusiano yao yalipoanzia.
Swali je Mariah na Nick wamerudiana?

Comments