Maneno matatu Zari amewaandikia wanae siku ya kumuaga aliyekuwa mume wake


Leo May 29 ni siku ambayo familia, ndugu, jamaa na marafiki wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda ambaye ni mume wa zamani wa Zari The Bosslady , Ivan Ssemwanga  ‘Ivan Don’ ambaye alifariki wiki iliyopita huko mjini Pretoria Afrika Kusini wameungana kuuaga mwili wa marehemu nchini Uganda.
Kupitia ukurasa wa Instagram Zari amepost picha wakati wanaelekea kanisani na picha nyingine alipost akiwa na watoto wake watatu aliowapata na Ivan na kuandika ‘I gat you’ Ikiwa na tafsiri ya kuwa ‘nipo nanyi’

Comments