Malaika: Sijawahi kutoka kimapenzi na DJ

Msanii wa muziki, Queen Malaika amesema si kweli kwamba alikuwa akitoka kimapenzi na Dj maarufu nchini kitu kilichopekea kuachana na mpenzi wake ambaye alikuwa akimsimamia kimuziki mara baada ya kuacha kufanya kazi na Chege na Adam Juma.
Malaika
Malaika akipiga stori na Show ya The Play List ya Times Fm amesema anawaheshimu sana Madj wote, na ni mara chache sana yeye kuonana na madj.
“Ilikuwa ni kawaida tu kama watu wanavyokuwa wana-date kusaidiana maisha, hakuwa meneja na hatukuwa na mkataba wowote. Kwanza hakuwa na mkwanja kama watu wanavyosema, alikuwa kawaida sana, nitakuwa muongo kwenye mahusiano kuna vitu kweli alikuwa ananisaidia kama mpenzi lakini hatukuendana tu tabia tukaachana,” amesema Malaika.

Comments