Majeruhi wa Lucky Vicent wanaotibiwa Marekani

Majeruhi watatu wa ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent waliowasili jana nchini Marekani, inaelezwa hali zao kiafya kuendelea vizuri.
Majeruhi hao kabla ya kuondoka nchini
Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amesema Doreen ameingizwa moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji, na Sadia na Wilson watafanyiwa upasuaji kesho.
“Madaktari wamemfanyia mtoto Doreen upasuaji wa bega, na nyonga kwa mafanikio, baadae leo mtoto Doreen anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa taya, mapema siku ya kesho mtoto huyu atafanyiwa upasuaji wa mgongo. Tuendelee kumweka yeye na wenzake katika maombi na sala zetu,” ameandika Nyalandu kwenye mtandao wa kijamii.

Comments