Hii ni ziara ya kwanza kwa Macron tokea achaguliwe kuwa Rais wa Ufaransa
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametaka kufanyika marekebisho makubwa ndani ya bara la Ulaya kufuatia maongezi kati yake na Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel mjini Berlin.
Katika ziara yake ya kwanza kama Rais, Macron amesema wamekubaliana kwa pamoja kufanya kazi ndani ya Umoja wa Ulaya kwa ukaribu zaidi.Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesema kutakua na hatua katika kuweka mambo sawa hususan masuala ya kodi.
Kabla ya kuelekea Ujerumani, Macron amemteua Edouard Philippe kuwa waziri mkuu mpya akitokea chama cha mrengo wa kati cha Republican.
Comments
Post a Comment