LIGI KUU KUENDELEA WIKIENDI HII KWA MICHEZO 6 KATIKA VIWANJA TOFAUTI

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea Jumamosi Mei 6 na Jumapili Mei 7, kwa jumla ya michezo sita. Kwa mujjibu wa ratiba, Jumamosi kutakuwa na michezo mitano na Jumapili kutakuwa na mechi moja.

Michezo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Toto African na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mwadui kwenye Uwanja wao huko mkoani Ruvuma.
Kagera Sugar itaalikwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Dar Young Africans ya Dar es Salaam itaialika Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo ya Jumamosi Mei 6, Azam FC itaialika Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam ilihali Jumapili kutakuwa na mchezo kati ya Simba SC na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, mchezo kati ya Azam na Mbao utakuwa 1.00 usiku.

Comments