Waziri wa habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harryson Mwakyembe ameweka baraka zake kwenye kampuni ya ku-bet ya SPORTPESA ambayo imetangaza kuingia rasmi Tanzania May 9 2017 ambapo wakati akiikaribisha akazungumzia na ishu ya kina Mbwana Samatta,
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Dk Harisson Mwakyembe ameipokea kwa mikono miwili kampuni ya kubashiri matokeo ya michezo kutoka Kenya ya SportPesa kwa kuihakikishia ushirikiano na Serikali ya awamu ya tano .
Mwakyembe amesema hii ni fursa nzuri sana kwa watanzania kwani SportPesa sio wamekuja kuwekeza tu kwenye mpira wa miguu bali wamekuja kuleta hamasa hata kwenye michezo mingine kama Ndondi,Rugby na riadha, hivyo Serikali kupitia wizara ya Michezo imewapokea na itawapa ushirikiano.Sportpesa ni Kampuni ya kwanza kubwa ya Kubashiri matokeo kutoka Afrika ambayo inadhamini Klabu ya Hull City inayoshiriki ligi kuu England, huku ikiwa na haki ya matangazo na vilabu vya Arsenal na Southampton.
Ujio wa Sports pesa nchini utavinufaisha vilabu vya Simba na Yanga ambavyo vipo mbioni kumwaga wino na kampuni hiyo ikiwa kama mwanzo tuu na baadaye kuendelea kudhamini klabu nyingine za ligi kuu Tanzania bara.
“Ujio wa SportPesa nchini Tanzania sio kwa sababu ya vilabu vya ligi kuu peke yake bali tutaingia mpaka kwenye timu ndogo kabisa mnaziita mchangani ?,,Hii yote ni kuleta hamasa kwenye soka letu nadhani mmejionea wenyewe Kenya walivyopiga hatua kwa miaka hii miwili kwenye soka“Alisema Abbas Tarimba Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania.
SportPesa wamezindua rasmi tawi lao nchini Tanzania leo na wametoa kiasi cha Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kuichangia timu taifa ya vijana Serengeti Boys.Tazama picha za Matukio mbali mbali hapa chini za uzinduzi wa SportPesa jinsi ulivyofana
Comments
Post a Comment