KIONGOZI WA ISLAMIC STATE NCHINI AFGANISTAN AUAWA



Wanajeshi wa Afghanistan wakisaidiwa na Marekani wamekuwa wakishambulia Islamic State karibuni
Wanajeshi wa Afghanistan wakisaidiwa na Marekani wamekuwa wakishambulia Islamic State karibuni
Kiongozi wa kundi la Islamic State (IS) nchini Afghanistan, Abdul Hasib, ameuawa, afisi ya Rais Ashraf Ghani imesema.
Taarifa kutoka kwa afisi hiyo imesema kiongozi huyo aliuawa siku 10 zilizopita katika operesheni ya kijeshi iliyoongozwa na wanajeshi maalum wa Afghanistan katika mkoa wa Nangarhar, mashariki mwa nchi hiyo.
Hasib anaaminika kuhusika katika shambulio la mwezi Machi katika hospitali ya kijeshi mjini Kabul, ambapo watu zaidi ya 30 walifariki.
Mwezi uliopita, wizara ya ulinzi ya Marekani pentagon ilisema kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba Hasib aliuawa katika operesheni ya kijeshi ya makomando wa Marekani an Afghanistan.
Aprili, jeshi la Marekani liliangusha bomu kubwa zaidi ambalo si la nyuklia kuwahi kutumiwa na taifa hilo.
Lengo la kuangusha bomu hilo lilikuwa kuharibu njia za chini kwa chini zilizodaiwa kutumiwa na IS katika eneo la Nangarhar.
IS walitangaza kuingia Afghanistan na Pakistan pale walipotangaza kuundwa kwa Mkoa wa Khorasan mwaka 2015, na tangu wakati huo wametekeleza mashambulio kadha. Julai 2016, waliua watu karibu 80 katika shambulio la kujitoa mhanga katika mkutano Kabul.
Nagharhar
Miezi mitatu baadaye, mashambulio mawili sawa katika sherehe za kidini za Ashura, yalisababisha vifo vya watu 30.
 
Na Novemba 2016, walishambulia msikiti Kabul na kuua watu 30.
IS pia walidai kuhusika katika shambulio la kujitoa mhanga Mahakama ya Juu Kabul mwezi Februari ambapo watu 22 walifariki.

Comments