KIJANA WA IRAN ANAYEFANANA NA LIONEL MESSI

Reza Parastesh ni kijana kutokea nchini Iran anayefananishwa na mwanasoka wa kulipwa kutokea nchini Hispania, katika klabu ya Barcelona Lionel Messi.

Reza Parastesh, mwenye umri wa miaka ishirini na tano kwa sasa, hivi karibuni ameanzisha mtindo wa ukataji nywele na kupunguza ndevu zake kama mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina . Hali inayopelekea watu wa mji wa Hamaden-Iran kumfananisha na nguli huyo ya mpira wa miguu.


Kijana huyo alianza kufananishwa na Messi miezi michache iliopita, baada ya kupiga picha akiwa amevaa jezi kama za mchezaji soka wa Barcelona namba 10 Lionel Messi. Kufuatia kufanana huko, watu wengi katika mji wa Hamaden wamekuwa wakiomba kupiga naye picha, kitu kinachopelekea msongamano wa watu kila atakapokuwepo.
Kwa kuyaona hayo, polisi wa eneo hilo wamelazimika kumchukua na kumpeleka katika kituo cha polisi mwishoni mwa wiki iliyopita ili kuondoa msongamano.

Kijana huyo amesema kuwa anafurahi kuona kila anapopita watu wanamfananisha na mwanasoka huyo, na pia anafurahi kuona akifurahisha watu hao.

Parastesh a.k.a Messi amekuwa akifanyiwa mahojiano ya mara kwa mara na vituo vya habari na kufanikiwa kusaini mikataba mikubwa ya uonyeshaji mavazi, na kwa sasa anafanya mazoezi makubwa ya kujua mbinu za mpira wa miguu ili akidhi vigezo kama vya Messi halisi.

Comments