Kiir amfukuza mkuu wa majeshi

Rais Salva Kiir
Rais Salva Kiir
               
Rais Salva Kiir wa Sudan kusini amemfukuza kazi mkuu wa Jeshi la nchi hiyo Jenerali Paul Malong.
Hakuna sababu yoyote iliyotajwa katika vyombo vya habari vya serikali, lakini katika siku za hivi karibuni maafisa wengi wa ngazi za juu wamekuwa wakijiuzulu na pia wengine kutoka serikali ya Sudan Kusini.
Mwandishi wa BBC anasema Jenerali Malong anaonekana na Wasudan wengi kama mtu mwenye nguvu, na wanasubiri kuona atakavyopokea kuondolewa katika nafasi hiyo.
Wengi wamekuwa na wasiwasi kuhusiana na upendeleo wa kikabila na uhalifu wa kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo yameiingiza Sudan kusini katika mgogoro uliodumu kwa miaka minne sasa.

Comments