Msanii mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Khadija Kopa amelijia juu Baraza la Sanaa Taifa (BATASA) kwa kushindwa kuulinda muziki wao.
Akiongea na mtangazaji wa Ice Fm ya Njombe, Gami Dee, malkia huyo wa mipasho amesema, wasanii wa muziki wa bendi wamekuwa wakiimba nyimbo zao bure kwenye mabaa bila idhini yao lakini BASATA imeshindwa kufanya lolote.
“Hawa viongozi sijui BASATA sijui nini? Sijui wanasimamia mziki wetu, hawatusimamii sisi tunanyimbo zetu na kazi zetu watu wanafanya bure baa nini bila idhini yetu sisi. Sisi wenyewe tunahangaika watu wanaenda baa, na kushuka kwa taarab ndio kushuka kwa mapato,” amesema Kopa.
“Taarab yetu wanaipiga kwenye mabaa bure, wanapiga kiingilio bia na wanaimba nyimbo zetu, sasa mtu anakua anajua mimi nikienda baa nitanunua bia moja nitasikiliza. Kitu kinachojihifadhi ndio kinatafutwa lakini kinachojitembeza hakitafutwi kwasababu wanajua ntakiona tu,” ameongeza.

Comments
Post a Comment