Katy Perry apata shavu katika msimu mpya wa American Idol

Katy Perry amechaguliwa kama jaji kwenye ujio mpya wa shindano la American Idol.

Muimbaji huyo wa Pop kutoka Marekani amekuwa jaji wa kwanza kutangazwa kupitia kituo cha runinga cha ABC ambacho ndicho kitaonyesha mashindano hayo.
Baada ya kutangazwa katika nafasi hiyo, Perry alisema, “Ninaona fahari na furaha kuwa jaji wa kwanza kurudi katika utamaduni wa American Idol wa kufanya ndoto kuwa kweli kwa vipaji vya ajabu kupitia watu maarufu na hadithi za kweli.”

“I’m always listening to new music, and love discovering diamonds in the rough – from mentoring young artists on my label, or highlighting new artists on my tours, I want to bring it back to the music,” ameongeza.
Naye Channing Dungey ambaye ni rais wa kituo cha ABC Entertaiment Group amemtaja Ryan Seacrest kuwa atarudi kwenye mashindano hayo katika nafasi yake ya utangazaji. Mashindano hayo yalisimama kwa muda tangu mwezi April mwaka jana ambapo yalikuwa yakionyeshwa na kituo cha runinga cha FOX.

Comments