Nahodha wa klabu ya Simba SC, Jonas Mkude ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Katika ajali hiyo Mkude , amepata michubuko katika baadhi ya sehemu ya mwili na hivyo kuruhusiwa hospitalini hapo alipokuwa akipata matibabu tangu alipo wasili siku ya hapo jana.
Mkude na watu wengine watano akiwemo dereva walikuwa kwenye Totota Land Cruiser V8 wakisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na walipofika Dumila tairi la mbele likapasuka na gari hiyo kupoteza mwelekeo hadi kwenye pori upande wa kushoto.
Abiria mmoja, Shose Fidelis alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro, wakati wengine, Jasmin na Faudhia wamelazwa hospitalini hapo, huku dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanae kwa jina la utani, Rais wa Kibamba anashikiliwa na Polisi.

Comments
Post a Comment