Jidenna atangaza hili baada ya kuzimiwa mziki jukwaani

Ikiwa zimepita siku chache baada ya msanii wa muziki kutokea Marekani ambaye ana asili ya kiafrika Jidenna kuzimiwa umeme katika showa kubwa ya One Africa Music Festival, Uingereza, Msanii huyo ameamua kuja na Tour yake mwenyewe.

Tour hiyo inayotarajiwa kuanza ifikapo mwezi Julai tarehe 20 na kumlizika Agost 27 mwaka huu, imepewa jina la “Long Live the Chief Tour’, ambayo imetokana na moja ya ngoma yake alioitoa mwaka huu.

Long live the chief tour inatarajiwa kuanza katiaka mji wa Raleigh na kumalizika katika mji wa Vancouver. Jidenna mwenyewe alitumia akaunti yake ya Twitter kuitangaza tour hiyo ikiwa kesho ndio tiketi zinatarajiwa kuuzwa.

Comments