India kufungua daraja refu mpakani na China

India kufungua daraja refu mpakani na India
India kufungua daraja refu mpakani na India
India itazindua daraja lenye urefu wa kilomita 9.15 linalopitia juu ya mto Lohit ,likiwa ndio refu zaidi nchini humo ambalo litaunganisha jimbo lenye utata la Arunachal Pradesh na kaskazini mashariki mwa jimbo la Tibet.
China hivi majuzi ilipinga mpango wa kumruhusu kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama kutembelea taifa hilo na pia imepinga utengenezaji wa miundo msingi ya kijeshi katika eneo hilo.
Lakini India imetetea haki yake ya kufanya hivyo.
''Huku China ikiendelea na ubishi huo ni wakati tunafaa kuimarisha miundo misingi yetu ili kutetea eneo letu'' ,alisema waziri wa mdogo wa maswala ya ndani nchini humo Khiren Rijiju ambaye ni mkazi wa Arunachal Pradesh .
Bwana Rajiju awali alikuwa amesema kuwa Arunachal Pradesh ni eneo la India na kwamba ukweli hautabadilika ''wapende wasipende''.
Ujenzi wa daraja hilo la la Dhola Sadiya ulianza mwaka 2011.

Comments