IDRIS SULTAN AMEANDIKA HICHI BAADA YA AJALI YA ARUSHA

Mchekeshaji Idris Sultan ameandika ujumbe mrefu na kuelezea hisia zake kuhusu vifo vya wanafunzi zaidi ya 30 wa shule ya Lucky Vicent mkoani Arusha.

Idris Sultan
 
 “Dear uliye hai na mimi leo, kuna aliyeamka asubuhi akiwa na ndoto ya kuwa lawyer, pilot, doctor, president, billionaire, baba, mama, mwalimu na hata kuwa raisi wa nchi hii. Wakati tukipanga yetu Mungu anapanga yake pia, kuna mama leo hii ni nesi na ameokoa watoto wa wenzake miaka zaidi ya 10 ila wa kwake hajapata nafasi hata ya kumsikia pumzi ya mwisho, kuna baba aliyetoka asubuhi kwenda kupigana amalize ada ya mtoto ambaye kampoteza bila taarifa wala kutarajia, kuna mama katoka tu kumuona mwanae na kesho yake ndio anaambiwa hatunae tena anatamani hata angemuambia jinsi gani anampenda hata mara ya mwisho.
“As much as painful this is right now naomba tusisahau kumuamini Mwenyezi maana ndiye pekee anayetupa na kuchukua, tutamuuliza kwanini nyingi, kwanuni unatupa makubwa ya moyo kama haya kwanini mtoto pekee uliyempa mama unamchukua ? Kwanini ulimpa ? Ulimpa ili umchukue ? Unatuadhibu au tumekosea mangapi yanayostahili haya ? Kwanini usitufanyie mengine na badala yake unachukua roho nyeupe za hawa watoto ambao hawajafanya hata theluthi ya makosa yetu sisi ? ila tukumbuke Mungu hajatuacha na yupo na sisi tumshukuru kwa kutuweka hai tuzuie vifo na ajali za barabarani zinazozidi kwa sababu ya uzembe ila tukumbuke pia wakati Mungu anawachukua hawa 36 kuna sehemu tofauti ameokoa zaidi ya 10,000 siku hiyo hiyo.
“Wazazi na ndugu mliopoteza leo Mungu hakupi majaribu asiyojua kama utaweza au utashindwa, together we will get through this, God bless you we love you. Mungu ibariki Tanzania, ni machache nisiyoweza kuyasema bila kutulia kila sentensi na chozi kunitoka. Let us be here for each other na tuombe tupewe siku njema yenye nguvu sio ya kusahau bali ya kuweza kuishi na kuwa na amani na hili,” ameandika Idris.

Comments