HUU NDIO UWANJA WA FAINALI ZA ASFC

Baada ya uwanja utakaopigwa mchezo wa Fainali ya FA kujulikana, wadau wa soka wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya mahala itakapofanyika kwa fainali hizo ambazo zinawakutanisha klabu ya Soka ya Mbao Fc dhidi ya Wakongwe wa ligi Simba Sc, katika fainali hizo za 2017 (Azam Sports Federation Cup),


Uwanja wa Jammhuri mkoani Dodoma, ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa fainali kati ya Simba vs Mbao, pambano linalotarajiwa kupigwa Mei 28, 2017.
Kwa mujibu wa kanuni, Simba ndio wenyeji wa mchezo huo kwa sababu ndio walikuwa wa kwanza kufuzu kucheza fainali kwa kuifunga Azam kwenye mchezo wa nusu fainali, kabla ya Mbao ambao waliifunga Yanga kwenye nusu fainali kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.


Kabla ya uwanja wa Jamhuri-Dodoma kutajwa kuwa ndio utatumika kwa ajili ya fainali ya FA Cup, kulikua na mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii ambapo wadau wa soka nchini walikuwa wakijadili tweet ya Rais wa TFF kwamba kutakuwa na droo ya kutafuta uwanja utakaotukika kwa ajili ya fainali hiyo.

Comments