HIKI NDICHO KINACHOMUWEKA BUSY RICH MAVOKO

Msanii Rich Mavoko kutoka lebo ya WCB, amesema kitu ambacho kinachukua muda wake mwingi kwa sasa ni maandalizi ya albam yake ambayo itakuwa ya kwanza tangu aanze muziki.
Rich Mavoko
Rich Mavoko alikiambia kipindi cha Top 20 cha Clouds FM kuwa, ikifika jioni saa 12 inabidi aende studio akafanye kazi hadi saa 12 asubuhi, hicho ndicho kitu pekee kinachmuweka busy kwa sasa.
“Hii itakuwa albam yangu ya kwanza kubwa kufanya, nilishawahi kutengeneza na watu wangu wa mwanzo ila haikufanikiwa kutoka,” alisema Rich Mavoko.

Comments