Haya ndiyo maneno 10 aliyoandika Kikwete baada ya kukutana na Samatta

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana usiku amekutana na nahodha wa Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta huko Ubelgiji alikoenda kwa ajili ya Mkutano wa kutatua migogoro ya kisiasa nchini Libya.
Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa na Mbwana Samatta
Mzee Kikwete mapema baada ya kukutana na nyota huyo anayekipiga kunako Klabu ya Genk alionesha furaha yake na kuandika ujumbe mzuri wa kufurahishwa kwa kukutana nae.
Mbwana Samatta akimkabidhi Jezi Rais Kikwete
Nikiwa hapa Brussels kuhudhuria Mkutano wa Wadau wa Libya nimepata fursa ya kukutana na mwanasoka na kipenzi chetu @samatta77 leo hii“, Ameandika Kikwete lwenye ukurasa wake wa Twitter.
Samatta nae hakuchukulia poa shavu hilo la kutembelewa na Rais Mstaafu kwa Kuandika “Ni wakati mzuri siku zote kukutana na our former president Mr @JakayaKikwete Wise and charming man. Asante sana mheshimiwa mungu akuweke” .
Mbwana Samatta ni moja ya wachezaji ambao wametajwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kuvaana na Lesotho mwezi ujao kwenye mechi za kufuzu AFCON.

Comments