Hamilton, ampigia saluti dereva wa Ferrari , Sebastian Vettel

Dereva wa mashindano ya Fomular 1, Lewis Hamilton, amempigia saluti dereva mwenzake ambae ni mshindani wake mkubwa katika mashindano ya Formula 1  Sebastian Vettel , nakusema kuwa ndie dereva namba moja katika kampuni ya  Ferrari .

                                     Dereva wa Mercedes, Lewis Hamilton
Vettel ameshinda katika mashindano ya  Monaco Grand Prix  baada ya kumshinda dereva mwenzake wa kampuni ya  Ferrari’ Kimi Raikkonen aliyekuwa anampa changamoto kubwa katika mashindano hayo.

Dereva wa Ferrari , Sebastian Vettel  akishangilia Ubingwa wake akiwa na dereva wa Red Bull,  Daniel Ricciardo 
“Ni wazi kuwa  Ferrari  wamepata dereva namba moja katika katika kampuni yao ” alisema Hamilton
“Ni vigumu sana kuiongoza gari na kuruka umbali mrefu vinginevyo timu ikupatie gari jingine la ziada” alisema Hamilton.
Dereva wa Ferrari , Sebastian Vettel , akiwa na timu yake katika mashindano ya Monaco Grand 
Hata hivyo dereva huyo wa kampuni ya Mercedes hakuomba kupatiwa mtu wa ziada wa kusaidiana naye kama ilivyo kwa  Valtteri Bottas.
“Sikuzungumza na timu yangu na sina mpango huo, Valtteri , anafanya kazi nzuri sana na katika wakati huu hatufikirii kuongeza mtu mwingine” alisema Hamilton.

Dereva wa Ferrari , Sebastian Vettel, akiwapungia mkono mashabiki

“Ni muhimu kukusanya  nguvu zetu kwa pamoja , kwa sababu kazi yetu ni kuhakikisha tunamshinda mshindani wetu ambae ni Ferraris na hicho ndio kitu kitakacho tuongezea thamani. Alisema dereva huyo wa kampuni ya Mercedes, ambae alishika nafasi ya saba katika mashindano ya Monaco Grand Prix .

Comments