Habari za usiku huu kuhusu Majeruhi wa ajali ya Wanafunzi Arusha


Tunafahamu Watoto watatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya basi la Wanafunzi Karatu Arusha walipelekwa Marekani kwa ndege maalum ambayo inafanya kazi kama Ambulance na walifika salama na kuendelea na matibabu chini ya Madaktari wazoefu.
Taarifa mpya za usiku huu kuhusu hali ya mmoja wao akiwa Hospitali ya Mercy, Sioux City IA ni kwamba Mtoto Doreen amemaliza kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo na Madaktari wamesema wamefanikiwa kwa ufanisi mkubwa kupita matarajio.
Doreen akiwa Hospitali, picha na maelezo ni kutoka kwa Mbunge Lazaro Nyalandu
Doreen alikuwa afanyiwe upasuaji kwa makadrio ya masaa matano na dakika 30 lakini zoezi hilo lilikamilika kwa masaa manne huku timu ya “Surgical Support” IKIWA na watu 6 na wakiongozwa na Madaktari bingwa wawili, Dr. Meyer na Dr. Durward.
Mtoto Doreen amehamishwa kutoka chumba cha upasuaji na kupekewa ICU na Madaktari wamesema kwasababu hali yake imeridhisha sana, baadae leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya upasuaji na kumrudisha wodi ya watoto.

Comments