Katika kuuendea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan imetangazwa good news iliyonifikia kutoka kwa Mwimbaji staa wa Bongofleva Shetta kwenda kwa mashabiki wake baada ya kuamua kutoa misaada kwenye Vituo vya Watoto wenye Uhitaji Tanzania nzima.
Kupitia account yake ya Instagram, Shetta ametoa mawasiliano yake kutoa nafasi kwa wahusika wa vituo hivyo ambao wanahitaji msaada ili aweze ku-share nao kitu kidogo alichojaaliwa kuelekea msimu huu wa Ramadhani: “Msimu wa Ramadhan unakaribia Mimi kama Shetta na menejimenti Yangu nzima napenda kukufahamisha kuwa kwa kidogo nilichonacho natarajia kuanza kusaidia na kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na wenye uhitaji mkubwa mikoa yote ya Tanzania ambayo Ntaweza kuifikia.
“Naamini Vipo vituo vingi vyenye uhitaji mkubwa sana wa mahitaji ya kila siku. Hivyo basi popote ulipo kama unajua au unahusika na kituo chochote usisite kuwasiliana nasi kupitia;
“Social media (Instagram, Twitter, FaceBook; @OfficialShetta or @MxCarter)
Email; shettamusic@gmail.com or MxCarter@slidevisuals.com
Simu; +255 22 278 0288 / 0655653030
Ili tuweze kukufikia kwa Urahisi Kabisa.”
Comments
Post a Comment