Filamu mpya ya kuchekesha anayoigiza Arnold Schwarzenegger….


China’s Bliss Media imepata haki za kutayarisha filamu ya kuchekesha ya Why We’re Killing Gunther, inayoigizwa na Arnold Schwarzenegger.
Filamu hii inahusu HitMan mkubwa duniani anayetaka kumuuwa HitMan mwenzake, mastaa wengine kwenye hii ilamu ni pamoja na Bobby Moynihan, Cobie Smulders, Paul Brittain, Ryan Gaul, Hannah Simone, Allison Tolman, Aaron Yoo, Amir Talai na Peter Kelamis.
Filamu hii inaongozwa na producer wa kipindi cha kuchekesha cha usiku maarufu Marekani kama Saturday Night Live , Bwana Taran Killam, itakuwa ni filamu yake ya kwanza.
Ni muda mrefu toka kumuona Arnold Schwarzenegger kwenye filamu ya kuchekesha….
 

Comments