Fareed Kubanda aka Fid Q amewashauri wasanii wenzake kuwekeza kupitia fedha wanazozipata kipindi hiki ambacho wanafanya vizuri kabla hawajaja hawajapotea.
Rapper huyo amemtolea mfano, Mr. Nice ambaye aliwahi kukubalika ndani ya Bongo na hata nje lakini leo hii hata mashabiki hawampi tena nafasi kama aliyokuwa nayo mwanzo.
“Hatuwezi kuishi kwa kutegemea show milele au kwa kuuza miziki tu, kila kitu kina muda, muda wake ukifika kinagoma. Hakuna kitu permanent, hata nguvu sio kitu permanent, nguvu aliyokuwa nayo Mr. nice yule wa “Kukukapanda baiskeli na bata kava laizoni” iko tofauti na aliyonayo hivi sasa au hata vipau mbele anavyopewa na wadau wake,” Fid amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One.
“Hapo kitakacho kubeba ni uzito wa carrier au chanel uliyojitengenezea katika kipindi fulani cha maisha yako, ili kuziakisi au kutoka droo na fursa ziletwazo na kujituma kwako mzigoni. Lakini pia kuna kitu kinaitwa trend ambacho hiki huja na huondoka, hivyo hivyo mashabiki leo wapo kwa Diamond kesho wapo kwa Alikiba na siku nyingine watakuwa kwa Bibi Cheka. Ili isikupe stress unashauriwa kuwekeza kwenye faida juu ya sasa au baadae, yote kwa manufaa ya baadae,” ameongeza.
Fid amesisitiza, “Tumia muda wako kwa kina kufanya utafiti wa fursa za kibiashara au hata wataalamu ambao watapelekea wewe kama msanii ukajikuta unanunua asset zenye potential ya kuongezeka thamani kwa kdri ya muda unavyokwenda na kujipatia income ya hapa na pale itakayopelekea uweze kujikimu vyema kimaisha na kusababisha akaunti yako ya benki iendelee kuwa nene kwa kipindi chote. Badala ya wasanii wakipata pesa na kukimbilia kununua magari yakifahari na nyumba . Ningeshauri tu invest hizo pesa na hayo magari ya kifahari na nyumba yatakuja tu baadae.”

Comments
Post a Comment