Daxo Chali akana kurudia beat kwa Dogo Janja na Madee

Prodyuza Daxo Chali amesema wimbo mpya wa Dogo Janja ‘Ukivaaje Utapendeza’ haufanani na ule wa Madee ‘Hela’, ila watu wanashindwa kuelewa kila prodyuza huwa na vionjo vyake katika beats.
Daxo Chali
Daxo Chali alipoulizwa na kipindi cha XXL cha Clouds FM, kwa nini beat ya wimbo wa Madee inakaribia kufanana na ya Dogo Janja. Prodyuza huyo alitolea mfano wa Dj Mustard, na kusema wakati DJ huyo anaanzisha style yake ya beat, kila mtu alikuwa anasema beat zake zinafanana lakini ndio ulikuwa utambulisho wake.
“So hii ni touch yangu, mimi natumia sana tarumbeta kitu ambacho maprduyza wengine hawatumii, ukiona tena nimetumia tarumbeta utaona kama muziki umefanana ila ni touch nyingine, codes nyingine na mizunguko mingine kabisa,” alisema.

Comments