Chuck Norris ataka kuwa boss wa FBI….



Kama Rais wa Marekani Donald Trump hana mtu wa kumpa kazi ya kuwa boss wa FBI ,basi muigizaji mkongwe wa filamu za ngumi Chuck Norris yupo tayari kuchukua kazi hio.
Akiwa jukwanii kutangaza biashara yake mpya ya maji ya chupa staa huyu amesema “Kama kuna mtu wa kusafisha anahitajika, basi niwe mimi, nitachukua kazi hio,
Chuck Norris, 77, aliunga mkono chama cha Donald Trump kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Kwa sasa Chuck Norris anatangaza bidha yake mpya ya maji ya chupa iliyopewa jina “CForce,”.

Comments