Rapa na DJ mwenye heshima yake kwenye game ya Hip Hop kutoka Marekani, DJ Khaled amenunua jumba la kisasa kutoka kwa msanii mwenzake Robbie Williams lililoko jijini Los Angeles, jumba hilo limenunuliwa na DJ Khaled kwa zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 21.
Ukiwa ndani ya mjengo huo utakutana na bafu 11, vyumba vya kulala 7, na uko kwenye eneo la ukubwa wa futi za mraba 10,681 na ulikuwa unauzwa kwa dola milioni 11 lakini Khaled aliomba punguzo na kuuziwa kwa dola milioni 9.9 za marekani ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 21 za kibongo.
Nimekuwekea hapa picha zote za mjengo wa rapa DJ Khaled ambaye pia ni mmiliki wa lebel ya We The Best Music Group.
Comments
Post a Comment