BRIGHT ALILIA PENZI LA VANESSA MDEE

Msanii Bright amefunguka na kusema kwamba msanii mwenzake, Vanessa Mdee asingekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Jux, yeye angemchukua mrembo huyo.
Bright na Vanessa Mdee
 
 
 
 
 
Bright amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kwamba, kuwa na Vanessa ni ndoto yake ya siku nyingi ila inashindwa kutimia kutokana na uwepo wa Jux.
“Unajua mawazo huwa hayafi ndio maana watu wanakufa na ndoto, mimi naamini kama itatokea lakini naona pale kuna mtu anang’ang’ana. Ila ikitokea fresha mimi namchukua, nitajiongeza,” amesema Bright.

 

Comments