Mmoja kati ya waasisi wa muziki wa Bongo Flava nchini, Boni Luv amefunguka jinsi walivyokuwa wanafanya kazi kipindi cha nyuma wakati muziki wa kizazi kipya unaanza nchini.
Akiongea na mtangazaji wa Ice FM, Gami Dee, Boni Luv amelinganisha ufanyaji kazi wa sasa na zamani nakuona tofauti kubwa iliyopo ni kipato pekee.
“Zamani tulikuwa tunarekodia wasanii nyimbo bure kabisa, mambo ya wasanii kutoa pesa ili warekodiwe yalianza mwaka 1995 na bei ya kurekodi ilikuwa elfu tano. Na hela yenyewe bado ilikuwa shida wasanii kuipata.”
Boni amefunguka pia kwa radio presenters na Djs kuwatoza pesa wasanii. “zamani tulikua tunafanya kazi na presenter ndio walikua wanatafuta kazi kutoka kwetu sisi lakini kwa sasa lazima uandae bajeti,” ameongeza.
Boni Luv amemtaja Omary Tambwe maarufu kama Lill Ommy ndio mtangazaji ambaye anakuja vizuri sana na anaejituma sana.

Comments
Post a Comment