Mapema baada ya kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho beki kisiki wa klabu ya Simba SC, Abdi Banda amewaaga rasmi mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo.
Banda kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram amethibitisha taarifa hizo za kuhama Msimbazi huku akiwaaga mashabiki wa Simba na kuwashukuru kwa ushirikisho waliomuonesha kwa kipindi chote.
“Ahsante mungu nashukur kwa hiki ulichotujaalia. Zawad ya mashabiki wa simba nawaachia acha na mm nitafute maisha sehem nyingine. Nitamiss vitu vingi hasa sapport yenu na moyo wenu wa uvumilivu ahsanten sana kwaherini“,ameandika Banda kwenye ukurasa wake wa Instagram .
Beki huyo Kinda ambaye katika mchezo wa jana aliingia na kuchukua nafasi ya beki wa kushoto baada ya Mohamed Zimbwe Jr kuumia kunako dakika ya 47 amechukua maamuzi ya kuikacha klabu hiyo ili kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.
Kwenye fainali hiyo ya jana ya Kombe la Azam Sports Federation Cup Simba walishinda goli 2-1 dhidi ya Mbao FC.
Comments
Post a Comment