ASLAY AWAPA SOMO KINA DADA

Msanii wa muziki kutoka Mkubwa na Wanawe, Aslay amedai wimbo wake mpya ‘Usiitie Doa’ ni maalum kwaajili ya kuwafunda akina dada ambao wanaingia kwenye maisha ya ndoa.
Muimbaji huyo ambaye ni baba wa mtoto mmoja, amesema ndani ya wimbo huo amevaa uhusika wa baba ambaye anamweleza mwanaye namna ya kuishi vizuri na watu.
“Wimbo ‘Usiitie Doa’ nimemwongelea msichana ambaye anaenda kuolewa, yaani nimekuwa kama namfunda japo kuwa namfunda kiume kama baba. Mwanangu ukienda huko ishi vizuri na mumeo, angalia maisha yako vizuri, fuatilia nyendo zako vizuri, ogopa marafiki wabaya,” alisema Aslay.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai hakuwa na mpango wa kumtumia Stan Bakora kwenye video ya wimbo huo.
“Stan ni mwanangu kinoma, wakati naangaika kutafuta nguo nilimfuata huyu jamaa akanitengenezea nguo kali sana. Pia akaniambia mimi nitakuwa kama mwanaume wa ukweli. Kwa hiyo jamaa amenionyesha upendo wa hali ya juu na namshukuru sana,”
Image result for ASLAY PICHA

Comments