Arsene Wenger hajui hatima yake Arsenal baada ya kombe la FA

Wenger alijiunga na Arsenal mwaka 1996
Wenger alijiunga na Arsenal mwaka 1996
Arsene Wenger hajui kama mchezo wa fainali wa kombe la FA utakuwa wa mwisho akiwa kama kocha wa Arsenal.
Raia huyo wa Ufaransa, ambaye mustakabali wake utaamuliwa na mkutano wa bodi baada ya mchezo huo, amekuwa Kocha wa timu hiyo tangu mwaka 1996 lakini mkataba wake utafikia ukingoni majira ya joto.
Siku ya Jumapili alieleza kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wake kuliathiri uwezo wa klabu msimu huu,lakini hakupenda kulizungumzia zaidi kabla ya mchezo wa Chelsea.
''nataka kushinda kombe kwa ajili ya klabu yangu, hicho tu ndicho nachokiangalia''
Wenger ameshinda mataji matatu ya Ligi kuu na sita ya FA katika kipindi cha miongo miwili lakini msimu huu amekabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mashabiki wakimtaka ajiuzulu.
Kutokana na kumaliza wakiwa nafasi ya tano kwenye michuano ya ligi kuu, washika bunduki hao wameshindwa kufuzu ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 20

Comments