App ya Wema Sepetu yarudi hewani Tena

Application ya simu janja ya Wema Sepetu (WS), hivi karibuni ilipata tatizo la kupotea hewani baada ya kuzidiwa na wingi wa mashabiki ambao walikuwa wakiingia kwenye mtandao huo.
Wema Sepetu
Martin Kadinda ambaye ni mtu wa karibu wa malkia hiyo wa filamu, aliiambia Bongo5 kuwa app hiyo ilipotea hewani baada ya watu wengi kuingia kwa wakati mmoja hali iliyosababisha kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Jumatatu hii muigizaji huyo amesema app hiyo imerudi rasmi hewani, hivyo mashabiki wake wanaweza kupata habari mbalimbali kupitia mtandao huo.
“Can i be your sunshine & moonlight…? 🤔🤔 Thank you Da Pendo for this amazing facebeat  Laviemakeup. You do a great job kwenye 📷 … Nawawekea 3 za mwisho… The rest mtazikuta app…. I told u guys we were having technical problems with issue ya malipo… Ryt… We have sorted that issue,” aliandika Wema Instagram alionyesha sample za picha ambazo zitapikana kwenye App hilo.
App hiyo inapatikana bure kabisa kwenye simu za Androids kwa kuingia playstore.

Comments