WAZIRI MKUU ATOA AGIZO HILI KWA MIFUKO YA UWEKEZAJI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo kwa mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuweka wazi majukumu yake kwa wananchi ili wanufaike na mifuko hiyo.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo Mjini Dodoma katika viwanja vya Mashujaa, wakati akizungumza na wakazi wa mji huo katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
“Sasa tujitambulishe na mifuko hii itumie nafasi hii kutoa maelezo sahihi ya mfuko na kazi zake kwa wananchi kuhusu shughuli wanazo zifanya, mikopo wanayoitoa ni lazima ijulikane na iwe ya wazi kabisa , vigezo vinavyozingatiwa katika kutoa mikopo hiyo na utaratibu mzima wa kupata uwezesho huo lazima uwe wazi,” alisema Waziri Majaliwa.
Aidha Waziri Majaliwa alitoa wito kwa wananchi kujitokeza na kuchangamkia fursa za kuwezeshwa na mifuko hiyo.
“Ukitaka kulima zabibu fedha zinapatikana katika vibanda hivi njoo, ukitaka kufuga njoo kwa hawa, ukitaka kulima mtama njoo kwa hawa na ukitaka matreka njoo yapo hapa chukua kalime na sisi tukisema tunatekeleza njoo uchukue mtaji kupitia taasisi zetu zote.”

Comments