WAZIRI MKUU AKAMILISHA UKAGUZI WA SHEREHE ZA MUUNGANO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya ukaguzi wa miundombinu kwa ajili ya sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema kuwa, maandalizi yake yako pazuri.


Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Jumatatu mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi na kukagua Uwanja wa Jamhuri ambapo sherehe hizo zitafanyika na uwanja wa Nyerere Square.
“Nimekuja kuangalia maandalizi ya sherehe hizo yamefikia wapi, najua kutakuwa na maonyesho ya kijeshi zikiwemo michezo na burudani kutoka Tanzania Bara za Visiwani,” alisema.
Hata hivyo Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi kutoka wilaya zote za mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani wafike kwenye maonyesho hayo ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania yanafanyika mkoani humo.
“Tunatarajia wageni wengi kutoka nje ya mkoa huu wakiwemo viongozi wastaafu wa kitaifa, waheshimiwa mabalozi na wake wa waasisi wa Taifa hili, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume. Pia tutawatambulisha rasmi ndugu zetu waliochanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964,” alisema.

Comments