Wabunge wa Uganda wamekosoa mipango ya rais Yoweri Museveni kuongeza idadi ya washauri wa kibinafsi wakisema kuwa fedha hizo zinaweza kutumiwa kununua vifaa vya hospitali mbali na kuongeza mishahara ya maafisa wa matibabu kulingana na gazeti la Observer.
Inadaiwa kuwa rais Museveni ametoa ombi la kutaka kuongeza washauri 18 na hivyo kuongeza idadi hiyo hadi washauri 163.Gazeti hilo linaripoti kwamba imekuwa utamaduni kwa rais Museveni kuongeza washauri baada ya uchaguzi wa urais ama baada ya kufanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.
Kulingana na sera ya 2017/18 ya rais,uteuzi huo wa washauri 18 wa rais utaongeza gharama ya washauri hao kufikia dola milioni 7.6.
Gazeti la Observer limemnukuu mbunge Mathias Mpuuga anayenshtumu rais kwa kutumia vibaya bajeti.
Kwa jumla kila mshauri atakuwa akipokea mshahara wa dola 631 pamoja na dereva atakayelipwa dola 53.
Comments
Post a Comment